Bi MUGABE ATEULIWA KUONGOZA ZANU-PF

Bi Mugabe ameteuliwa kuongoza kitengo cha wanawake katika ZANU-PF
Mkewe rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameingia katika uongozi wa chama tawala cha Zanu-PF .
Grace 49 ameteuliwa kuongoza kitengo cha wanawake cha Zanu -PF ,wadhfa atakaochukuwa rasmi mwezi Desemba katika kongamano la kitaifa la wanachama wa ZANU-PF.
  Cheo hicho kitamruhusu Bi Mugabe kushiriki katika mikutano ya kamati kuu ya chama hicho ambayo ni yenye shinikizo kubwa katika uendeshaji wa taifa hilo la kusini mwa Afrika.
Kumekuwa na mvutano na taharuki kubwa katika chama cha Zanu-PF kufuatia kuzorota kwa Afya ya rais Mugabe katika miaka ya hivi karibuni na haijulikana ni nani atakayemrithi kiongozi huyo wa Zimbabwe.

  Bi Grace ni mke wa pili wa rais Robert Mugabe
Bi Mugabe atahudumu kama katibu mkuu wa kitengo cha wanawake baada ya kuteuliwa katika mkutano wa kamati kuu iliyofanyika mjini Harare.
Bi Mugabe alikuwa wakati mmoja msaidizi wake rais Mugabe kabla hawajoana mwaka wa 1996.Wamejaliwa watoto watatu .Rais Mugabe 90,alihudhuria kikao hicho .Bwana Mugabe ametawalataifa hilo tangu itwae uhuru wake mwaka wa 1980.








Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment