Hatimaye dalili za safari ya mwisho ya marehemu Albert Mangwea kurejea nyumbani zimeanza kuonekana.
Tayari mwili wa Mangweha ‘Mangwea’ umetolewa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya St Helen Joseph na kukabidhiwa kwa undertaker.
Undertaker ni mtu anayefanya kazi ya kushughulikia kumuosha, kumvisha nguo na kumpamba maiti na baadaye kumhifadhi vizuri kwenye jeneza.
Kampuni inayofanya kazi hiyo tayari imeuchukua mwili wa Mangwea na hiyo ni dalili kwamba ndani ya siku mbili safari ya kurejea nyumbani itakuwa imeiva.
“Tayari undertaker ameuchukua mwili, hali hiyo ina maanisha kwamba safari ya Dar ni ndani ya siku hizi mbili.
“Vijana hapa wanaendelea na michango na wengine wataungana na mwili wa marehemu kuja huko nyumbani,” alisema Mtanzania anayeishi nchini Afrika Kusini aitwaye Joseph.
“Nimeambiwa huyo undertaker ni Mtanzania, hivyo tunaamini mambo yataenda vizuri zaidi,” aliongeza Joseph.
Tayari imeelezwa mwili wa Mangwea utawasili nchini Jumapili jioni na Jumatatu ataangwa kabla ya kuanza safari ya kwenda Morogoro ambako atazikwa.
Mangwea alifariki Jumanne iliyopita baada ya kukutwa akiwa chumbani ameishakufa, huku mwenzake M To The P akiwa taabani, hadi sasa yuko hospitali.
0 comments:
Post a Comment