Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakitoa msaada wa madawa mbalimbali kwa Hospitali ya St Elizabeth mbele ya Dkt Thomas Kway, Mganga Mkuu wa hospitali hiyo (koti jeupe). Mwenye shati jekundu ni Mustapha, Mkurugenzi wa Bushbuck Safaris.
ARUSHA -- SERIKALI NA WADAU WA UTALII WAMETOA VIFAA NA MADAWA MBALIMBALI VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 18/- ILI KUSAIDIA WALIONUSURIKA KWA BOMU LILILOLIPULIWA KATIKA ENEO LA KANISA LA PAROKIA TEULE YA MTAKATIFU JOSEPH MFANYAKAZI HUKO OLASITI MKOANI ARUSHA SIKU YA JUMAPILI, 05.05.2013.
PAMOJA NA MSAADA HUO, PIA WAMEAHIDI KUANZAISHA MFUKO WA MANUSURA HAO KWA MINAJILI YA KUWASAIDIA BAADA YA MATIBABU, NA KWA KUWANZIA WAMEKUSANYA KIASI CHA SH. MILIONI 100.
"TUNATARAJIA KUANZISHA MFUKO WA WAHANGA UITWAO VICTIM FUND UTAKUWA UKISAIDIA MAJERUHI WAKATI WAKIWA HOSPITALI NA BAADA YA HAPO TUTAENDELEA KUSAIDIA HADI WATAKAPOWEZA KUENDELEA NA MAISHA YAO. KWA KUANZIA MFUKO WETU UTAKUWA NA KIASI CHA SHILINGI MILIONI MIA MOJA," ALISEMA MUSTAPHA, MKURUGENZI WA BUSHBUCK SAFARI YA JIJINI ARUSHA.
WAKIKABIDHI KWA PAMOJA VIFAA HIVYO, NAIBU WAZIRI - MALIASILI NA UTALII, LAZARO NYALANDU ALISEMA KUWA VIFAA HIVYO NI MWANZO WA KUSAIDIA MAJERUHI HAO NA HOSPITALI YA ST. ELIZABETH KWANI NDIYO HOSPITALI TEULE YA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA INAHITAJIKA KUSAIDIWA KWA WAKATI HUU ILI IWEZE KWENDANA NA KASI YA WAGONJWA WANAOFIKA HAPO.
MKUU WA MKOA MAGESA MULONGO ALISEMA KUWA SERIKALI MAZIKO YA WALIOFARIKI KUTOKANA NA MLIPUKO WA BOMU YATAFANYIKA KWENYE MAENEO YA KANISA LA MTAKATIFU JOSEPH MFANYAKAZI SIKU YA IJUMAA. AMESEMA WANATARAJIA WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA ATAONGOZA WAKAZI WA JIJI HILO KWENYE MAZIKO KWA NIABA YA SERIKALI.
MBUNGE WA ARUSHA MJINI, GODBLESS LEMA ALISEMA ANAWAPA POLE MAJERUHI NA WAFIWA NA KUTAKA WAJIPE MOYO WA SUBIRA WAKATI HUU WA MAJONZI HALI AKIWATAKA WAKAZI WA JIMBO LAKE KUWA KITU KIMOJA KWENYE SUALA HILI BILA KUJALI TOFAUTI ZAO ZA KISIASA.
MAKAMPUNI MBALIMBALI YAMEKUWA YAKIJITOLEA VIFAA MBALI MBALI KWA MAJERUHI HAO. KAMPUNI ZILIZOTOA MISAADA MBALIMBALI SIKU YA LEO NI PAMOJA NA KITUO CHA MIKUTANO CHA KIMATAIFA (AICC), VIOLA SAFARIS, SHIRIKA LA MSALABA MWEKUNDU, NGORONGORO CONSERVATION AUTHORITY, BUSHBUCK SAFARI NA HIDDEN VALLEY SAFARIS LTD ZOTE ZA JIJINI ARUSHA.
VIFAA VILIVYOTOLEWA NA WADAU HAO NI PAMOJA NA MAGODORO, MABLANKETI, MADAWA YA AINA MBALIMBALI, ROZARI, VITABU VYA MAFUNDISHO YA IMANI NA VITENGE.
AKIPOKEA VIFAA HIVYO, MGANGA MKUU MFAWIDHI WA HOSPITALI HIYO, DKT. MLAY ALISEMA VIMEKUJA WAKATI MUAFAKA KWANI HOSPITALI INAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWEMO CHUMBA CHA WAGONJWA MAHUTUTI (ICU) HIVYO AKAWATAKA WADAU KUSHIRIKI KATIKA KUSAIDIA UJENZI WA WODI HIYO YA WAGONJWA MAHUTUTI.
0 comments:
Post a Comment