WAZIRI MKUU WA SYRIA AJIUNGA NA MAGEUZI

Waziri mkuu wa Syria Riad Hijab, amejiuzulu kutoka serikali ya rais Bashar al-Assad na kujiunga na harakati za mageuzi.
Bwana Hijab aliteuliwa kwa wadhifa huo chini ya miezi miwili iliyopita na kujiuzulu kwake kunamfanya yeye kuwa afisaa wa ngazi ya juu zaidi kujiuzulu kutoka kwa serikali ya Assad,
Inaarifiwa familia yake pia imekimbia kutoka Syria.
Riad ambaye ni muumini wa madhehebu ya Suni, anatoka eneo la Deir al-Zour mashariki mwa Syria, eneo ambalo limenaswa katika vita vinavyoendelea vya kumng'oa madarakani rais Assad.
Taarifa kutoka kwa msemaji wake , Mohammed el-Etri amesema kuwa yeye na familia yake wako salama nchini Jordan.
Habari zinasema kuwa hatua hii ni dalili ya serikali ya Assad kuonekana dhaifu na kuwa hata wakuu wa majeshi wanaaza kupata shinikizo la kuondoka.
Pia waasi wanasema mawaziri wengine wawili wa serikali ya rais Assad pia wameasi.
lakini wanasema waziri wa fedha, Mohammad Jalilati alikamatwa alipojaribu kutoroka.
Mwezi mmoja uliopia, Brigedia Generali Manaf Tlas, aliyesemekana kuwa mshirika wa karibu sana wa rais Assad pia alijiuzulu.
Majenerali wengine thelathini wamesemekana kuvuka mpaka na kuingia nchini Uturuki.
Hata hivyo kuna tetes kuwa waziri mkuu huyo alifutwa kazi ingawa serikali ya Syria haikutoa taarifa zozote kuelezea hatua ya kumfuta kazi.
Omar Ghalawanji, ndiye atachukua nafasi yake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment