TAARIFA RASMI KUHUSU HUSSEIN MACHOZI KUREJEA TETEMESHA

Hii ni taarifa rasmi kwa media HUSSEIN MACHOZI na kurejea katika wadau wote kuhusiana na familia ya TETEMESHA RECORDZ, iliyomtengeneza na kumkuza kimuziki mpaka hapo alipo toka mwaka 2007.Kumekuwa na taarifa nyingi hapo katikati lakini hii ndio taarifa rasmi na ya kweli kuwa yalitokea matatizo kidogo mwaka jana (2010) mwanzoni, yaliyotokana na Hussein kukiuka baadhi ya masharti ya mkataba wake na Tetemesha, yaliyopelekea uongozi kuamua kusitisha kwa muda mkataba wake ili kumpa nafasi ya kupewa nguvu msanii mwingine aliyekuwa ndio anaaza kutambuulishwa mwaka jana anayefahamika kama SAGNA. Baada ya kumtambulisha vizuri Sagna, mwaka huu pia Tetemesha tumeweza kumtambulisha msanii mwingine wa tatu aitwaye C-SIR MADINI. Sasa tumeona ni wakati muafaka wa kumrudisha Hussein Machozi rasmi ndani ya Tetemesha baada ya kukaa nae chini na kufanya makubaliano mapya na kusaini mkataba mwingine toka katikati ya mwaka huu, isipokuwa tumechelewa kuwapa taarifa kwasababu tulikuwa tunaweka kwanza mambo kadhaa sawa.

NEW SONG:Hussein Machozi akiwa chini ya Tetemesha Entertainment ameshaanza kurekodi baadhi ya nyimbo mpya zitakazotoka mwaka ujao 2012, lakini kwa sasa tunautambulisha wimbo wake ambao ni REMIX ya wimbo alioutoa mwaka jana unaitwa “UNANIFAA”.

Katika version ya mwanzo ya wimbo huo aliimba peke yake, lakini katika remix hii amewashirikisha wasanii wenzake wa Tetemesha ambao ni C-sir Madini na Sagna.

Unanifaa remix imeandikwa na Hussein mwenyewe verse yake na chorus, na verse za Sagna na C-sir zimeandikwa na mwandishi rasmi wa Tetemesha anaitwa JOSEFLY kwa kushirikiana na Kid Bwoy.

Version ya mwanzo ya wimbo huo ilifanyika Akhenato Records chini ya Lil Ghetto. Remix beat imefanywa na Amba, na vilivyosalia vyote vimefanyika Tetemesha Recordz.

CREDITS:

Artists: HUSSEIN MACHOZI FT. C-SIR MADINI & SAGNA

Song title: UNANIFAA (REMIX) Written by: Verse-1: JOSEFLY, Verse-2 & Chorus: HUSSEIN MACHOZI, Verse-3: JOSEFLY & KID BWOY

Produced by: AMBA for TETEMESHA RECORDZ 2011

Vocals Recorded by: KID BWOY

Mixed by: KID BWOY

CONTACTS:Hussein Machozi 0718 877728

Kid Bwoy 0713 131073

Thanx for the support. T

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment