TUMPIGE TAFU YA SHULE MWANAMUZIKI BEN PAUL

Alimaliza shule Mwaka jana February kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Azania
Mwaka huu ndio anataka kujiunga na chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM lakini hana ada ya kulipa kwa mwaka mzima pale chuoni.Albam yake imetoka iko mtaani na ndio pekee anayoitegemea iuze apate pesa za kulipia chuoni kwa Mwaka huu.


Kama ilivyo kwa wanamuziki wengi wa hapa Tanzania wenye uwezo mkubwa wa kuimba wametokea familia za kimasikini.Ben Paul ni mtoto wa pili katika familia ya watoto wanne wa kwanza alishafariki.Anaishi eneo la airport hapa Dar es salaam katika familia ya maisha ya chini kabisa.Baada ya kumaliza shule mwaka jana aliusucrifise ili kufanya mziki utakao mpa pesa ya kulipa ada maana nyumbani wazazi hawakuwa na kitu.


Ana kipaji cha kuimba na anapenda kusoma na ndio maana amefanikiwa kumaliza kidato cha sita tofauti na wanamuziki wengine ambao walikimbia shule ili kufanya muziki.Baada ya kutoa albam Mwaka huu ameamua kuinadi ili kukusanya ada ambayo deadline ni tarehe 31 mwezi huu.Ada inayotakiwa ni Tsh 1,200,000 ila ameweka target ya kupata Tsh 2,400,000 kwa ajili ya miaka miwili.


Mimi binafsi nimeguswa sana na juhudi zake binafsi za kutaka kurudi shule na njia anayoitumia kuuza albam yake.Albam hii inauzwa katika style ya mnada na ilianzia katika kipindi cha XXL leo.Nimenunua albam yake moja kwa Tsh 50,000 hivyo mdau wangu naomba tuungane katika kununua albam hii kwa uwezo uliojaaliwa wewe ili tumkusanyie kijana wetu pesa hii.Kama upo tayari piga namba hii 0787 583132 ili kuweka oda na kusema utainunua kwa shilingi ngapi lakini sio chini ya 20,000 maana muda umeenda sana.


Albam hii ina nyimbo 10 zikiwemo nikikupata,samboira,maumivu,maneno,maboma,ninaringa akiwa na Lina na nyingine.Kiukweli kijana anaimba sana tu pia usikose kusikiliza leo tena kesho.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment